Facebook Comments Box

Saturday, August 30, 2014

VIONGOZI WA SHURA YA MAIMAM WAMTEMBELEA DR SLAA

Viongozi wa Shura ya Maimam leo asubuhi wamemtembelea Dr. Slaa ofisini kwake iliyopo mtaa wa Ufipa Kinondoni. Lengo la ziara hiyo ni
kumweleza Dr. Slaa juu ya udhalilishaji wanaofanyiwa Masheikh 19 wanaotuhumiwa kwa kesi ya Ugaidi wakiwa chini ya vyombo vya
sheria.

Hivi karibuni imeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa Mashekh hao wamekuwa wakidhalilishwa kijinsia na kuharibiwa sehemu za siri. Viongozi hao wamemwomba Dr. Slaa na Chama chake kuwaunga mkono katika kupaza sauti juu ya udhalilishaji huo na kumwomba ushirikiano katika maswala ya kisheria hasa ikizingatiwa kuwa CHADEMA ni wahanga wa matukio hayo ya udhalilishaji kwa vijana waliobambikwa kesi za ugaidi


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU