''Tunaipongeza timu ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani kwa kuchukua ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani majuzi (Aprili 6
mwaka huu) baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali
uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Ushindi kwa timu hiyo ni fahari kwa Tanzania, lakini kubwa ni kwa
kituo cha Mwanza ambacho ndicho kinachoiendesha pamoja na
wadhamini na wafadhili walioiwezesha kushiriki fainali hizo kwa
mara ya pili mfululizo.
Vilevile ushindi huo unatoa changamoto kubwa kwa wadau wa
mpira wa miguu kuwa watoto wa mitaani ni sehemu tu ya vipaji
vilivyotapaa nchini, hivyo iliyopo ni kuvisaka na kuvibaini vipaji
hivyo kwa ajili ya ustawi wa mchezo huo nchini.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tutaendelea
kushirikiana na kituo hicho cha Mwanza, na vingine vyote ambavyo
vinajishughulisha na mchezo huu, lengo likiwa ni kuundeleza na
hata kutoa ajira kwa vijana hapo baadaye kupitia mpira wa miguu.
Timu hiyo imerejea nchini leo ambapo imetua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 9 na nusu jioni kwa ndege
ya Emirates''
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog