Ngassa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria.
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa amepata zali Afrika, baada ya kumaliza kinara wa mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, licha ya klabu yake kuaga mashindano hayo katika mzunguko wa pili. Ngassa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria.
Ni baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufikia tamati wikiendi iliyopita na ES Setif kutangazwa mabingwa wapya wakibebwa na bao la ugenini kutokana na matokeo ya sare bao 1-1 mchezo wa Algeria na sare mabao 2-2 mchezo uliochezwa Kinshasa.
Ngassa aliyafunga mabao hayo katika raundi ya kwanza walipocheza na Komorozine ya Comoro mchezo wa kwanza walishinda 7-0 na marudiano walitoka kifua mbele kwa mabao 5-2.
Yanga ilitolewa kwenye mashindano na Al Ahly ya Misri kwa penalti 3-4. Lakini Ngassa hawezi kupewa zawadi yoyote kwavile wamefungana na kiutaratibu hata mchezaji akishinda tuzo hiyo CAF huwa haitoa zawadi.
Yanga ilitolewa kwenye mashindano na Al Ahly ya Misri kwa penalti 3-4. Lakini Ngassa hawezi kupewa zawadi yoyote kwavile wamefungana na kiutaratibu hata mchezaji akishinda tuzo hiyo CAF huwa haitoa zawadi.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog