Kabla ya kuwepo MuM alikuwa ni mhitimu wa Chuo cha Ualimu cha Kiislamu Ubungo Islamic Teacher's College ambako alihitimu mwaka 2004 na kisha akasomesha Msamala Muslim Songea na baadae Matangini Islamic Dar, akajiunga na
Chuo cha Waislamu Morogoro wakiwa ndio Batch ya mwanzo 2005. Baada ya kuhitimu alichaguliwa kuwa Mhadhiri Msaidizi na mwaka mmoja baadae alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamili na kurejea MuM ambako amekuwa akifanya kazi mpaka mauti yalipomkuta.
Bro. Alianza kupata mtihani wa maradhi mwaka 2011 na 2012 au 13 aligundulika kuwa na Maji kwenye mapafu waislamu wakachukuwa jukumu la kumpeleka India kwa matibabu akafanyiwa upasuaji na tatizo likapungua alirejea Alhamdulillaah ingawa alionekana wazi kuwa tayari amedhoofika, hakuwa Siraji yule handsome tuliyekuwa tukimjua.
Bro. Katika uhai wake ukiacha kwamba alikuwa superbright kitaaluma na kihoja na aliyekuwa na khofu ya dhati kwa Mola wake alikuwa role model, and very inspiring, fasaha na mtulivu sana asiye na papara katika mambo yake na huu ni sehemu ya urithi aliyotuachia.
Bro. Siraji alikuwa mtu huru na anayenyoosha maneno alipokuwa akisimamia haki, Kipindi cha mwangaza wa jamii Radio Iman na wasikizaji wake watashuhudia kwa hili na watasikitika sana kipindi hiki kumkosa huyu Akhy.
"Hao ni umma umekwishapita, wao wana malipo yao nanyi mna malipo yenu wala hamtoulizwa wao wamefanya nini (Bali mtaulizwa ninyi mmefanya nini) 2:141
Bro. Siraji ameacha mke na watoto wawili wa kiume. Tunaamini wajibu wake kwa jamii ya waislamu na watanzania kwa jumla ameutekeleza kikamilifu na hivyo anastahiki akapumzike.
Sisi sote ni wa Allaah na kwake ndio Marejeo. Allaah amsamehe madhambi yake amrehemu na ampe makazi mazuuri peponi.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog