Facebook Comments Box

Wednesday, September 24, 2014

ARSENAL YATOLEWA KOMBE LA LIGI HUKU LIVERPOOL IKIENDELEA

Wachezaji wa Southampton wakishangilia moja ya bao lao.

Timu ya Arsenal imetolewa katika kombe la Ligi baada ya kufungwa mabao 2 kwa 1 na Southampton, mchezo ambao umemalizika usiku huu.

Southampton ambayo inaendeleza mwanzo mzuri wa msimu baada ya kutoka nyuma kwani Arsenal ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Alexis Sanchez pale alipotandika mkwaju wa faul umbali wa mita 25 kwenye ukuta wa Southampton na kuandika bao la kuongoza kwa timu yake.

Lakini southampton walisawazisha makosa yao kwa kufunga bao baada ya mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Dusan Tadic kutokana na rafu aliyochezewa Debutant Sadio Mane. Nathaniel Clyne aliipatia timu yake bao la pili katika kipindi cha pili na kuibuka washindi.
 Tadic akifunga mkwaju wa penati.
 goli la pili kwa washindi.
 Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akilalamika.
Sanchez akiifungia Arsenal bao pekee katika mchezo huo.

Liverpool yenyewe imeendelea na hatua ya nne ya michuano hiyo baada ya kutoka sare ya 2 kwa 2 na Middlesbrough na Liver kushinda kwa penati 14 kwa 13.
 



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU