Facebook Comments Box

Monday, September 29, 2014

MALINDI YALIFUMUA BENCHI LAKE LA UFUNDI BAADA YA KUCHEZA MECHI MBILI TU


Kocha  Abdulghani  Msoma  na  kocha  msaidizi  Rashid  Lato  wakiwafatilia  kwa  karibu  vijana wa  Malindi.
 Klabu  ya  malindi  ya  mjini  Unguja  imeliongezea  makali  benchi  lake  la  ufundi  lililokuwa  likiongozwa  na  Mohamed  Said  Shubery  al  maarufu  Babu  Shube  na  badala  yake  sasa  litakuwa  likiongozwa  na  makocha  watatu  na  si wawili tena  na  wamemuongeza  kocha  Abdulghani  Himid  Msoma  katika kuinoa  timu hiyo  inayoshiriki  ligi  kuu  ya  Zanzibar  inayofahamika  kama  Grand malt  premier  league.
 
Uamuzi  huo  wa  malindi  umekuja  kufuatia  matokeo  mabaya  waliyopata  katika  mechi  zao  mbili  za ligi  walizocheza  na  mpaka  sasa  kuwa  hawana  hata  point  moja  ila  wameambulia  magoli  mawili  tu  uongozi  umeamua  kumuongezea  nguvu  za  kiufundi  kocha  huyo  mwenye  maneno  mengi  mfano  wa  kocha  Chelsea  ya  Uingereza  Jose  Mourinho, Mohamed  Shubery  au  Babu. Leo  asubuhi  alionekana  yuko  samba samba  na  kocha  Msoma na  pamoja  na  msaidizi wake  Rashid  Lato katika mazoezi ya mwisho Katika  uwanja  wa  Amaan  kabla  ya  mchezo  wa leo.
 
 Kocha   Msoma  aliyeanza  kazi  hiyo  ya  kuwanoa  Malindi  juzi  asubuhi  Kwenye  uwanja  wa  Amaan  na  jana  kuendelea  na  mazoezi  hayo  asubuhi  mtihani wake  wa  kwanza  ulikuwa   ni  leo  ambapo  Malindi  ilishuka  dimbani  kupepetana  na  timu  ya  Polisi  ya  Zanzibar  kwenye  uwanja  wa  Amaan  katika  mchezo  uliochezwa  saa  10  Alaasiri  umeshuhudiwa  Malindi  ikiibuka  na   ushindi  wa  goli  moja  kwa  nunge  dhidi  ya  maafande  hao  Polisi  Zanzibar, Malindi  sasa  baada  kuonja  ushindi  huo  hii  leo  angalau  sasa  wana  point  tatu  na  magoli  matatu.
.Malindi  wakiwa  katika  mazoezi  jana  asubuhi  ktk  uwanja wa Amaan.




HUKU NISSAN NYEUSI KULE BMW NYEUPEEE MBONA MNATUCHANGANYA?

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akijiandaa kukata keki yake ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Kijitonyama.

Wema Isaac Sepetu akiongea na wageni wake (hawapo pichani) kabla ya kukata Ndafu.
Martin Kadinda akimuonesha Wema Sepetu kadi ya gari.
Gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa Wema Sepetu na mpenzi wake Diamond Platnumz.Gari aina ya BMW alilozawadiwa Wema Sepetu na meneja wake Martin Kadinda.


SOMA MAGAZETI YA LEO TAREHE 29 SEPTEMBA 2014




Sunday, September 28, 2014

UTURUKI WARUHUSU HIJJAB KWA WANAFUNZI

Nchi ya Uturuki imeondoa marufuku ya kuvaa Hijabu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari iliyodumu takribani kwa muda wa muongo mmoja.

Uamuzi huo ulitangazwa siku ya Jumanne na Naibu Waziri Mkuu Bulent Arinc.


Akizungumza na waandishi wa habari Bulent Arinc alisema kwa sasa serikali imeruhusu wanafunzi kuhudhuria shuleni wakiwa wamevaa Hijabu katika shule zote zilizo chini ya Wizara ya
Elimu.

Bulent Arinc ambaye ni msemaji pia wa chama cha Justice and Development (AK) alisema agizo hilo baada ya siku mbili litakuwa lenye kutekelezwa baada ya kupeleka taarifa za kimaandishi katika Wizara husika.


Hijabu ilipigwa marufuku mwaka 1980 kwa wanafunzi, wafanyakazi katika taasisi za umma na serikali muda mfupi baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Tangu wakati huo wanawake waliokuwa wakivaa hijabu nchini humo walilazimika kuacha kazi katika ofisi za serikali.

Utawala wa Uturuki umekuwa ukijaribu kuwa mbali na taratibu za kiislamu kwa ajili ya kuridhisha nchi za Ulaya ili kuingizwa katika
umoja wa nchi hizo. Uturuki kwa muda mrefu imetaka kuwa mwanachama wa nchi hizo
za Ulaya bila mafanikio.

Waziri Mkuu ErdoÄŸan aliahidi kuondoa marufuku yote juu ya uvaaji wa Hijabu wakati aliposhinda kwa mara kwanza mwaka 2002.


Tangu wakati huo aliondoa marufuku ya kuvaa Hijabu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Hata hivyo bado vazi la Hijabu halijaruhusiwa kwa majaji, waendesha mashtaka, maafisa wa kijeshi na wafanyakazi wa kijeshi.

 Cha kuzingatia ni kuwa katika baadhi ya nchi za ulaya ikiwemo uingereza vazi la hijjab linavaliwa na watu wote hata askari kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.




MATOKEO NA PICHA YA MECHI ZILIZOCHEZWA JANA TANZANIA

Golikipa wa Polisi Morogoro, Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo September 27,2014.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akishangilia bao aliloifungia timu yake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi ya Morogoro uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ramadhani Singano 'Messi'
Timu ya soka ya Simba SC imelazimishwa sare ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni hii Septemba 27,2014,kufungana bao 1-1 na Polisi Morogoro Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Hiyo ni sare ya pili mfululizo kwa kocha Mzambia, Patrick Phiri baada ya wiki iliyopita kutoka 2-2 na Coastal Union Uwanja wa Taifa, licha ya kuongoza 2-0 hadi mapumziko. 




Hadi mapumziko, tayari Simba SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 32 akimalizia pasi fupi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. 


Timu ya Polisi inayofundishwa na Mohammed ‘Adoph’ Rishard ilibadilika na kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa Simba SC ambapo Danny Mrwanda, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, aliisawazishia Polisi baada ya kumzidi mbio na maarifa beki Joseph Owino kabla ya kumchambua vizuri kipa Hussein Sharrif ‘Cassilas’. 


Azam FC imepata ushindi wake wa pili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting leo kwenye Uwanja wa Chamazi. 
 

Azam FC ambao walianza ligi kwa kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 3-1, imeshinda mabao hayo mawili leo, yote yakitupiwa kimiani na Mrundi, Didier Kavumbagu ambaye sasa ana mabao manne. 
 


Matokeo mengine ya Ligi Kuu Vodacom 2014/2015 ni kama ifuatavyo:- 

Azam FC 2 - 0 Ruvu Shooting 

Mtibwa Sugar 3 – 1 Ndanda FC 

Mbeya City 1 – 0 Coast Union 

Mgambo Shooting 0 – 1 Stendi United


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU