Facebook Comments Box

Sunday, August 24, 2014

WAZEE WA MADRID WAWAONESHA WAZEE WENZAO WA TANZANIA KUWA MPIRA NI KAMA BAISKELI UKIJUA UMEJUA




Tanzania eleven na wageni wao Madrid walipokuwa uwanjani jana.
Mdau wa Kitongoni akiwa jukwaani kupata burudani hiyo hapo jana.
Heka heka langoni mwa Tanzania eleven 

kitongoni Taifa:

Mechi ilikuwa nzuri kila timu ilicheza vizuri japo real Madrid walionekana wana mazoezi na hawana vitambi kwa kuwaangalia ni wazee ila mpira wanaucheza vizuri. Mpira ni kama basikeli ukijua umejua tu.

Kwa upande wa Tanzania eleven Kalimangonga Ongala na Athuman china walicheza vizuri na walionekana kuisumbua sana ngome ya wazee wa madrid maana kuna wakati Kalimangonga alitolewa ikabidi arudishwe Maana timu ilipwaya.

Kwa upande wa makipa wote wawili Mohamed Mwameja na Peter Manyika walidata vizuri na wanaonesha bado ni hazina kubwa kwa Taifa letu maana ujuzi hauzeeki bwana asikwambie mtu.

Ila jambo nililojifunza katika mtanange ule ni kwamba Wazee.wetu wana akili ya mpira na control kuliko vijana wa sasa maana vijana mambo mengi mpira unataka vitu vitatu tu Control, Pass and Move mambo mengine ya nini.




Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU