Na Mwandishi Wetu,
WENGI
wa watu nchini China wanapendelea ujenzi wa majengo makubwa ya
kihistoria na magari kadhaa yenye muonekano wa alama ya uchina kama
ishara ya kuonyesha ufanisi wao katika uvumbuzi wa vitu mbalimbali
duniani.
Lakini
basi tena, wachina ni watu katika jamii wanaopenda kufanya mambo
makubwa na tofauti na ni wazalishaji wa vitu vingi vya hapa leo duniani,
sasa wachina wanatengeneza meli kubwa kwa mfano wa meli maarufu ya
Titanic.
Meli
ya Titanic iliyozama mwaka 1914 karibu karne moja iliyopita na kuua
watu karibu elfu moja, sasa kampuni kutoka uchina ya Star Investment
Group katika mkoa wa Sichuan itatumia dola za kimarekani 165 milioni
katika kujenga upya meli mfano wa Titanic.
Meli
hiyo mpya ya wachina itafanana kabisa na meli ya Titanic iliyozama
vibaya kwenye kina cha bahari karne moja iliyopita. Meli hiyo itajengwa
kwa ushirikiano na kampuni ya serikali ya China Ship building
Corporation ya Wuchang inatumika kama sehemu ya hifadhi ya makumbusho
katika mkoa wa Sichuan.
Katika
meli hii ya replica ni ishara ya uvumbuzi uliotukuka kutoka kwa wachina
na watazamiwa kuingiza mamilioni ya fedha kama riba kutokana na alama
ya Titanic duniani.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog