Facebook Comments Box

Saturday, October 26, 2013

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA OFISI ZA AZAM TV


Waandishi wa Habari wa vituo mbali mbali vya Televisheni pamoja na magazeti wa hapa Jijini Dar es Salaam  siku ya Jumamosi tarehe 26/10/2013 walipata fursa ya kutembelea ofisi za Azam Tv zilizopo Tazara.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media, Rhys Torrington akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media,Rhys Torrington akionyesha King'amuzi cha Azam TV kwa baadhi ya Waandishi wa habar.
Baadhi ya Wakuu wa vitengo mbalimbali vya kampuni ya Azam media wakimsikiliza Mkurugenzi wao.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Azam Media, Loth Mziray (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya Waandishi wa habar.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Azam Media Kitengo cha huduma kwa Wateja wakiwajibika.
Meneja Uzalishaji na Ufundi wa Kampuni ya Azam Media, Mehboob Al-Addad akionyesha moja ya mixer za sauti zilizopo ndani OB Van ya Azam TV ambayo ni ya kisasa na yenye vigezo vya kimataifa.
Wazee wa Kazi ndani ya OB Van la Azam Tv,toka kulia ni Meneja Uzalishaji na Ufundi wa Kampuni ya Azam Media, Mehboob Al-Addad, Meneja wa Azam FM na Matukio ya Moja kwa Moja,Yahya Mohamed pamoja na Fundi Mitambo wa OB Van hiyo, Saleh Mansoor aliyekaa wakifatilia moja ya kazi zao.

 OB Van ya Azam Tv



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU