Picha na Maktaba:
Matumizi ya dawa za kulevya nchini yamechukua sura mpya, baada
ya kubainika kuwa watumiaji wengi wa dawa hizo aina ya heroin na cocaine
sasa wanatumia dawa za hospitali zenye uwezo wa kulevya kuwa mbadala.
Watu wanadhani dawa za kulevya ni heroin na cocaine pekee, lakini
vijana wanavuta petroli, gundi, dawa za maumivu na za kifua ambazo zina
codeine, vyote hivi vinaathari,”
Matumizi hayo mabaya yamebainika kutokana na
kuwapo ongezeko la matumizi ya dawa za hospitali zilizo na nguvu
inayoelezwa kulingana na dawa za kulevya zikiwamo heroin, cocaine na
amphetamine.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Uhalifu na Dawa za
Kulevya (UNODC) ya mwaka 2013, inathibitisha ongezeko hilo la matumizi
ya dawa hizo, ambazo kitaalamu zinaitwa ‘new psychoactive substances
(NPS).
“Dawa mbadala za dawa za kulevya zimezua wasiwasi
mkubwa siyo kwa sababu ya ongezeko la matumizi yake, bali hata ukosefu
wa utafiti wa kisayansi na uelewa wa matumizi yake,” ilisema sehemu ya
ripoti ya UNODC.
Katibu Mkuu UNODC, Yury Ferdotov alieleza katika
ripoti hiyo ya hali ya dawa za kulevya mwaka 2013 kwamba, changamoto
kubwa iliyopo katika kudhibiti dawa hizo duniani ni matumizi ya dawa za
hospitali na kemikali zinazotumika kuzitengeneza kutumika kama dawa za
kulevya.
Alisema nchi nyingi duniani hazina sheria wala
uelewa kuhusu kemikali hizo, jambo linalosababisha wafanyabiashara
wakubwa kuendelea kusafirisha kemikali hizo au kutumia teknolojia kulima
mimea inayotumika kutengeneza dawa hizo.
UNODC limefafanua kuwa matumizi mabaya ya dawa
hutokea wakati dawa za hospitali zinapotumika kwa malengo mengine
kinyume na tiba.
Chanzo: Gazeti Mwananchi
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog