Facebook Comments Box

Thursday, September 5, 2013

WAKAZI WA DAR ES SALAAM KUENDELEA KUSOTA NA FOLENI ZA BARABARANI


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wataendelea kukumbwa na kero ya msongamano wa magari barabarani baada ya mpango wa serikali wa kupunguza tatizo hilo kupitia ujenzi wa barabara zilizopo nje ya jiji kukwama kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo wakandarasi wanaojitokeza kuomba kujenga kuomba  kiasi kikubwa.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale, alisema mpango huo wa kujenga barabara za nje ya jiji upo ingawa unakabiliwa na changamaoto mbalimbali zikiwamo watu kutojitokeza kuomba kazi ya kujenga na wanaojitokeza kuomba kiasi kikubwa cha fedha hatua iliyoifanya serikali kurudia kutangaza tenda.

Katika mkutano wa Bunge la bajeti mwaka huu, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alitangaza kwamba kwa  mwaka 2013/2014 serikali itajenga barabara za nje ya jiji la Dar es Salaam ili kukabiliana na msongamano wa magari.

Alizitaja kuwa ni pamoja na inayoanzia Mbezi Beach Tangi Bovu hadi Mbezi Shamba kupitia Goba, Mbezi Shamba hadi Tegeta kupitia Goba na ile ya Mbezi Shamba hadi Uwanja wa Ndege kupitia Kinyerezi.

Ahadi nyingine aliyotoa Dk. Magufuli kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014 ni ujenzi wa barabara za juu katika maeneo ya Tazara, Mwenge na Ubungo mipango ambayo mpaka sasa haijaanza kutekelezwa.

Wakati ahadi hizo zikichelewa kuanza, Tanroads  imesema barabara hizo zitajengwa kwa kiwango cha Lami na nyingine Changarawe kulingana na upatikanaji wa fedha.

Kuhusu bomoa bomoa mbalimbali zinazoendelea jijini Dar es Salaam, Mfugale alisema baadhi hawahusiki nazo na kutoa mfano nyumba zilizomolewa wiki iliyopita eneo la Mbezi Beach.

Alisema wananchi wakiona Tingatinga linabomoa mahali popote wanajua ni Tanroads na kusema kuwa baadhi ya maeneo yanabomolewa kwa ajili ya kupitisha bomba la maji au shughuli zingine za serikali siyo lazima iwe ujenzi wa barabara.

SOURCE: NIPASHE


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU