Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani (Picha zote, maelezo na video: IKULU)
Rais Jakaya Kikwete amempongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed
mwenye umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa kunyakua ubingwa
wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko
Orlando, Marekani, mwezi uliopita.
Kijana huyo, ambaye awali alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo, Dar es Salaam, alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya Afrika Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu.
Mwenyekiti wa Sport Training Centre (TSTF), Dennis Makoi amesema kuwa walipotambua kuwa kijana huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. Alisema kuwa walipata

mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki kituo cha kufundishia mchezo
huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani Desemba mwaka jana kwa
ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili huyo alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480 kutoka timu 44 kutoka nchi 14 ambapo jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.
Amy Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania ili kuukuza ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini kwao na kuitangaza Tanzania.
Hamisi Mohamed alisema anashukuru kwa malezi aliyoyapata katika kituo hicho cha watoto yatima cha Dogodgo Centre na kwa msaada waliojitolea katika kukiendeleza kipaji chake.

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Hamisi Mohamed. Kulia ni mfadhili wa
kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais Kikwete ni Sister Jean
Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha Dogodogo Centre
Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na
wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika
mashindano ya dunia
Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.
Rais Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na
kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote
katika michezo ya kimataifa
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog