
Yawezekana Taifa Stars ikawa haifanyi vizuri kwenye michuano ya 
kimataifa kiasi cha kuwa chini kwenye chati za soka barani Afrika na 
duniani kwa ujumla lakini jina la Taifa hili limekuwa likitajwa na lina 
uhakika wa kutajwa katika level za juu za soka barani afrika, hii ni 
kutokana na makubwa yanayofanywa na kijana mwenye umri wa miaka 21 raia 
wa Tanzania ambaye ni Mbwana Samatta .
Mchezaji huyu ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji amekuwa akifanya
 vizuri sana kwenye klabu yake ya Tp Mazembe ya Nchini Congo DRC kwenye 
michuano ya kimataifa na amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye michuano 
ya kombe la shirikisho barani Afrika .
Samatta alifunga bao moja kwenye mechi iliyochezwa juzi kati ya timu 
yake ya Tp Mazembe na FUS Rabat ambapo Mazembe ilishinda 3-0 na mpaka 
sasa Samatta amekuwa akifunga kwenye mechi zote nne za michuano hiyo 
ambazo Mazembe imecheza hali inayomfanya awe na nafasi kubwa ya kuwa 
mfungaji bora wa michuano hiyo wakati ikimalizika baadaye mwaka huu.

Mbwana
 Samatta akiwa anasaini Autograph za mashabiki wa soka Ivory Coast ambao
 walivutiwa na uwezo wake wakati wa mazoezi ya Taifa Stars nchini humo.
Samatta ambaye Mazembe ilimsajili toka Simba Sports Club ya Tanzania 
ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na amekuwa na rekodi 
nzuri sana ya kufunga karibu kila mechi ambayo anacheza kwenye klabu 
hiyo .
Samatta amefanya watanzania wengi kuwa na shauku ya kufahamu matokeo 
ya timu ya Tp Mazembe ambapo mara zote watu huuliza timu hiyo imeshinda 
au la na baada ya kuuliza hivyo huuliza tena Samatta amefunga mangapi 
kwa kuwa wana uhakika juu ya uwezo wake na rekodi yake ya kuzifumania 
nyavu.
Ubora wake umemfanya kuishi maisha ya kistaa akiwa nchini Kongo 
ambapo mashabiki wa Mazembe wanampenda kiasi cha kutaka kupiga naye 
picha kila wamwonapo mtaani na wakati mwingine kutaka kusukuma gari lake
 wanapoliona
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog