![]()  | 
| Arusha. | 
Maripota wawili wa millardayo.com kutoka Arusha wanaripoti 
kwamba mabomu ya machozi yakipigwa na Polisi yameanza kusikika toka saa 
kumi jioni kwenye eneo la Soweto.
Mmoja wa maripota hawa amesema wakati alipokua karibu na 
mkusanyiko huo kuna Askari Polisi mmoja ambae alijichanganya na kuingia 
katikati ya wafuasi wa Chadema ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu 
wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa kwa mabomu na kufariki June 15 
2013 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
Baada ya hapo hawa Wafuasi hawakupenda kitendo cha Polisi 
kujichanganya nao hivyo ikazuka kama kutoelewana huku wakitaka atoke, 
baada ya dakika kadhaa huku pia Viongozi wa Chadema wakihutubia…. ndio 
mabomu yakaanza kusikika.
Ripota wa pili anasema “Baada ya Tundu Lissu wa Chadema 
kuhutubia na kusema chanzo cha vifo vya June 15 2013 ni Polisi, yani 
vifo hivyo viliratibiwa na RPC Arusha… mabomu ya machozi ndio yakaanza 
kulipuliwa”
Mpaka saa kumi na moja na dakika 40 hii post inaingia hapa, 
wafuasi wa Chadema bado wako maeneo ya Soweto Arusha, wamegoma kuondoka 
na kusema wanataka kujua kwanza usalama wa Viongozi wao…. lakini pia 
mabomu yanaendelea kusikika kwenye sehemu nyingine kama Sanawari, Arusha
 mjini, Mianzini na maeneo mengine.
SOURSE: MILLARD AYO 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
