
Jeshi
 la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na 
maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu 
kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea 
kwenye viwanja hivyo .
Akizungumza
 ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema 
kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo  limeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu 
upelelezi.
Hali
 kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi 
wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya 
kuomboleza ..
Hata
 hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo 
hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA ,
 hali iliyoleta  mvutano kati ya
 viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja  alijichanganya na kuingia 
katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu 
wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu 
Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi 
kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, 
baada ya dakika kadhaa 
mabumu yalianza kusikika.
Baadhi
 ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa
 jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog