Facebook Comments Box

Monday, March 18, 2013

HANS POPPE AKATAA KURITHI MIKOBA YA RAGE


 Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba aliachia madaraka yake yote ndani ya kilabu hicho cha simba Nd Zacharia Hans Poppe amekataa kurithi madaraka aliyopewa na wanachama 698 wa kilabu hicho waliofanya kikao na kumpindua mwenyekiti wao Nd Aden Rage alioko india kwa matibabu.

Alipopigiwa simu na kuelezwa habari hizo Zacharia Hans Poppe, kwanza alisema hana taarifa za Mkutano huo wala yaliyofikiwa.

“Sina taarifa na wala siafiki, kwa sababu hakuna mtu aliyeshauriana na mimi kabla, na pia wamefanya mambo kinyume na Katiba,”alisema Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

“Lazima wanachama wawe na subira, wasubiri Mwenyekiti arudi aitishe mwenyewe Mkutano, yeye mwenyewe (Mwenyekiti) alikwishasema ataitisha Mkutano, sasa kitu gani kinachowafanya wao wanakosa subira,”.

“Mbaya zaidi wamekwenda kufanya Mkutano wao na kufikia maamuzi yao, bila hata kunitafuta kuniuliza kwanza, sasa hii si ni dharau? Ina maana wao wanataka mimi nifanye wanavyotaka wao, mimi sitaki kuwa sehemu ya migogoro katika Simba,” alisema Hans Poppe.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU