- Inawezekana kuwa imetekwa nyara
- Au Haitambui majukumu yake.
Wale wanaofahamu dhana nzima ya kuanzishwa Kamati ya Maridhiano
Zanzibar umefika wakati wa kujiuliza IKo wapi kamati ya Maridhiano?
Amma kwa wale wasiofahamu dhana na chimbuko la kuanzishwa kamati ya maridhiano wao watasema kamati hii ipo.
Ni vyema kufahamu chimbuko la dhana ya Kuweko Kamati ya Maridhiano.
Baada ya miongo ya misuguano ya kisiasa Zanzibar juhudi kadhaa
zilichukuliwa kurudisha imani miongoni mwa Wazanzibar ili kuendeleza
siasa chini ya misingi ya demokrasia, haki, usawa, pamoja na kutii
sheria za nchi huku tukidumisha usalama, umoja na amani.
Juhudi zilizaa matunda mwaka 2009, baada ya maridhiano yaliyofikiwa
baina ya vyama vya CCM na CUF na kuamua kufuta uhasama yaliyosimamiwa na
wajumbe kutoka pande zote mbili. Mwanzoni yalikuwa mazungumzo
yaliyoendeshwa kwa siri kubwa hadi pale ilipofika time ya kuyatangaza,
viongozi wakuu wawili waliyabariki, kuyakubali na kuyaridhia.
Kilichofuata ilikuwa ni “Road map” kuelekea dhamira thabiti ya
maridhiano haya ikiwa ni pamoja na kuliomba Baraza la Wawakilishi
kujadili dhana nzima, pale itakapoonekana inawafiki maridhiano haya
yasimamiwe kikatiba. Halkadhalika maamuzi yote lazima yasimamiwe na
wananchi wenyewe kwa kupiga kura ya maoni kukubali au kukataa.
Hivyo basi, Kamati ile iliyoasisi maridhiano ilikabidhisha mamlaka
yake kwa Baraza la Wawakilishi. Wakati wa mjadala, Baraza la Wawakilishi
liliunda kamati, ambayo ndio iliyosimamia hadi kuhitimisha maridhiano
na kuikaribisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Hapo utaona hadi kukamilika kwa maridhiano kulitokana na kamati
mbili; i) kamati ya kuasisi maridhiano na (ii) kamati ya kusimamia
maridhiano.
Hapa ndio dhana ya kuendelea kuwa na Kamati ya Mridhiano ilipoanzia.
Kuona kwamba ili Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar iweze kudumu na
kutatua vikwazo vitakavyojitokeza lazima kuwe na upande mwengine (third
party). Upande huu utakuwa suluhishi wa mizozo pindi ikijitokeza.
Vilevile utakuwa ndi muelekeo (dira) kuielekeza serikali pamoja na kuwa
kunganishi kwa wananchi.
Kwa vile haya ni maridhiano bila ya shaka kulikuwa na uhasama, hivyo
suala la usuluhishi na kusameheana lilipaswa lipewe nafasi yake.
Kuorodheshwa na sera za kitaifa na kutengwa zile sera za kivyama ilikuwa
ndio uti mgongo wa Kamati ya Maridhiano.
Haya yote yalitakiwa kufanywa na ile kamati iliyoundwa na Baraza la
Wawakilishi kwani imetokana na chombo cha kutunga sheria, imechaguliwana
wananchi pia inajumuisha wajumbe kutoka vyama vyote viwili (CCM na
CUF).
Kinyume chake ile kamati ya Waasisi ndio iliyojichukulia na
kujitwisha kama ndio Kamati ya Maridhiano. Hili limepelekea kukosa
utendaji na kupoteza muelekeo wa dhana nzima ya kuwa na Kamati ya
Maridhiano.
Kuna haja ya kufikiria kuundwa upya wa Kamati ya Maridhiano ili iweze
kufikia lengo la kuweko kwake. Zanzibar inahitaji sera za kitaifa,
umoja, suluhu (reconciliation), nani mwengine kama sio uimara wa
Kamati ya Maridhiano.
SOURSE: MZALENDO NET
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog