Facebook Comments Box

Tuesday, December 24, 2013

WANNE WAKAMATWA NA HEROIN ARUSHA


GEDSC DIGITAL CAMERAKamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari bunduki aina ya SMG iliyokamatwa wilayani Ngorongoro hivi karibuni huku mkono wake wa kulia akiwa ameshika kifurushi chenye madawa ya kulevya aina ya Heroin yaliyokamatwa jana wilayani Arumeru. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
 
Kuelekea katika kusherehekea Sikukuu ya Krimas, Jeshi la Polisi Mkoani hapa limeendelea kupambana na wahalifu wa madawa ya kulevya ambapo safari hii limefanikiwa kuwakamata watu wanne wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin. Tukio hilo limetokea jana tarehe 23.12.2014 muda wa saa 12:30 jioni maeneo ya Elikyurei wilayani Arumeru.
 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas amesema kwamba tukio hilo limefanikiwa baada ya kupata taarifa toka kwa raia wema ambapo askari wa Jeshi hilo walikwenda katika eneo husika na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa ndani ya chumba cha mtuhumiwa mmojawapo huku wakiwa wanaendelea kufunga kete za madawa hayo na tayari walikuwa wamefunga kete 25.
 
Kamanda Sabas aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Seifu Bakari (28) na Hamid Makame wote ni wakazi wa Elikyurei wilayani Arumeru pamoja na wenzao ambao ni Evance Gidion (29) Mkazi wa Ngarenaro na Abraham Hamis (23) Mkazi wa Kaloleni jijini hapa.
 
Kamanda Sabas alisema kwamba madawa hayo yenye uzito wa gramu 100 yanakadiriwa kuwa na thamani ya Tsh 10 Mil. Mpaka hivi Jeshi hilo linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili kufahamu undani zaidi na watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
 
Kufuatia tukio hilo na mengine ya nyuma Kamanda Sabas alizidi kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kwa jinsi wanavyoonyesha ushirikiano kwa jeshi hilo juu ya kufichua vitendo vya uhalifu na wahalifu na kuahidi kuendeleza falsafa ya Polisi Jamii ambayo inaleta mafanikio makubwa katika suala zima la kuimarisha amani na utulivu Mkoani hapa.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU