Facebook Comments Box

Wednesday, December 11, 2013

MANJI KUTOGOMBEA TENA UENYEKITI YANGA: YANGA YAPATA KATIBU MKUU MPYA

Mwenyekiti wa Young Africans Yusuf Manji leo amemtambulisha rasmi Bw. Beno Njovu kuwa katibu mkuu mpya wa klabu akichukua nafasi ya Lawrence Mwalusako aliyekua kaimu katibu mkuu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji amesema Beno Njovu anaanza kuitumikia hiyo nafasi mpya kuanzia leo na Mwalusako atakua nae pamoja kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka atakapokabidhi kazi rasmi.
Aidha Manji ametangaza mkutano mkuu wa wanachama Januari 19,2013 ambapo wanachama watapata fursa ya kupitia mapato na matumizi,  na ajenda zingine mbalimbali ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo.
Kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki kimemteua Bw.Seif Ahmed "Magari" kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa na kutokana na nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji wa klabu ya Yanga. 
Katika mkutano na wandishi wa habari makao makuu ya klabu Manji ametangaza rasmi kutogombea tena uenyekiti katika uchanguzi mkuu ujao, hili nimeliamua mwenyewe binafsi bila shinikizo na kikubwa nimefuata demokrasia.
Nina miezi saba kabla ya uchanguzi mkuu mwakani hivyo sasa ninajitahid kukamlisha shughuli zote ambazo nilianza kuzifanya ndani ya Yanga nikiwa kama mwenyekiti ili uongozi mpya utakaoingia uweze kuendeleza mipango ya kuifanya Yanga iwe klabu bora Tanzania.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU