Facebook Comments Box

Wednesday, December 11, 2013

ABIRIA WA TRENI YA MWAKYEMBE WAANZA KUPITIA MADIRISHANI HEBU JIONEE KATIKA PICHA HAPA

Na Kamera ya kitongoni Blog:
 
Treni inayobeba abiria katika Jiji la Dar es Salaam maarufu kama Treni ya Mwakyembe ambayo inafanya safari zake kutoka Stesheni katikati ya Jiji hadi Ubungo - Maziwa. Imejizolea umaarufu mkubwa katika kuwasaidia abiria wengi wanaopata taabu ya usafiri katika Jiji hili.

Kadri siku zinavyozidi kwenda usafiri huu wa treni umekuwa unapendwa sana na watu walio wengi japo hauwasaidii watu wote ndani ya Jiji hili kutokana na sababu kwamba hauna foleni hivyo kuwafanya watu walio wengi kuwahi kufika nyumbani kwao ukilinganisha na usafiri mwingine wa gari ambapo umekuwa na foleni kila kukicha.

Kutokana na kupendwa huko na watu walio wengi usafiri huu sasa umeanza kuwa wa taabu sana kwa abiria kupanda pindi safari inapotaka kuanza Stesheni. 

Baadhi ya abiria wamekuwa wakipitia madirishani kama ambavyo tumezoea kuona kwenye baadhi ya mabasi ya kubeba abiria maarufu kama 'daladala' hapa Dar es Salaam kama walivyokutwa na Kamera ya Kitongoni hapo jana siku ya Jumanne tarehe 10/12/2013. 
Abiria wakiwa wamepanga foleni kabla Treni haijafika Stesheni.
Abiria huyu kama unavyomuona hapa akilipigia dirisha hesabu ili apande na kulifanya dirisha ndiyo mlango.


Baada ya kulitathmini dirisha Jamaa aliweza kupanda na kama anavyoonekana akiingia kupitia dirishani na huu sio ustaarabu kabisa.
Abiria wastaarabu wakipanda Treni hiyo kupitia mlangoni kama wanavyoonekana hapo.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU