Facebook Comments Box

Thursday, November 21, 2013

MAHAKAMA YAMUHUKUMU KWA KOSA LA KUZAA MTOTO MWENYE SURA MBAYA.

Jian Feng amemshitaki mkewe kwa kumzalia binti mwenye sura mbaya. Mwanaume huyo aliiambia mahakama kuwa alimuoa mkewe kwa mapenzi ya dhati na waliishi kwa amani muda wote lakini matatizo yalianza baada ya mtoto huyo kuzaliwa.

Aliambia mahakama kuwa ilibidi afanye hadi kipimo cha DNA ili kuhakikisha kuwa mtoto huyo ni wake na vipimo vilitoa majibu ya kuwa ni wake.

Mwanamke huyo aliiambia mahakama kuwa kabla ya kukutana na mmewe huyo alifanyiwa upasuaji uliomgharimu zaidi ya fedha za kimarekani $ 100, 000 (laki moja) katika nchi ya Korea ya kusini ili kuupata urembo huo ulio mvutia mwanaume huyo.

Mahakama ili kuamuru mwanamke amlipe mwanaume fedha za kimarekani $ 120, 000 (laki moja na elfu ishirini) kwa kumzalia binti huyo mwenye sura mbaya





Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU