Facebook Comments Box

Saturday, November 2, 2013

ELIZABETH MICHAEL 'LULU' ATOA MSAADA WA FEDHA KWA WAGONJWA WA SARATANI OCEAN ROAD


Lulu atoa msaada wa fedha hospitali ya ocean road kwa wagonjwa wa Cancer.
Mwanadada Elizabeth Michael 'Lulu' ametembelea hospitali ya Ocean Road Iliyopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa zawadi za fedha kwa wagonjwa wa saratani hospitalini hapo.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Lulu ameandika "Naamini Mimi sio mwema sana mpaka Mungu akaniwezesha kuona mwezi huu nikiwa mzima na mwenye afya...! kwa kutambua Hilo nimeanza mwezi huu kwa kupita ktk hospital ya Ocean Road na kutoa mchango ili kuwasaidia wagonjwa wa Saratani.

Tuwe na utaratibu wa kuwakumbuka wahitaji kwa chochote tulichonacho! Nawatakia mwezi wenye Baraka na mafanikio!...

Kumbuka kutoa ni moyo na sio utajiri mtu yeyote anaweza kutoa kwa kadri alivyo jaaliwa na M/Mungu lakini halazimishwi na mtu ni wewe mwenyewe ukijiona unaweza unatoa na sio Ocean Road peke yake, kwani wahitaji wapo wengi sehemu nyingi iwe hospitali, vituo vya yatima na kwingineko.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU