Facebook Comments Box

Wednesday, October 9, 2013

MISHAHARA YA WAZIRI MKUU, MAWAZIRI NA RAIS WATAJWA

Picture
Zitto Kabwe: "Siku ya Nne ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetupeleka Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora. Nikiwa na Wenyeviti wa chama wa mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora pia Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi Ndg. Mambo tumefanya mikutano 4."
Mishahara ya Viongozi wa Umma lazima iwe wazi kwa umma. Sheria za Mishahara ziweke wazi kabisa kuwa mishahara hii itakuwa wazi na itakatwa kodi. Juzi Mpanda nimewaambia wananchi Mshahara wa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa mwezi. Nikiwa Igunga mnamo tarehe 13 Oktoba tutawaambia wananchi mshahara wa Rais na Makamu wa Rais. Iwapo Rais wa marekani mshahara wake na mapato yake ni wazi na unakatwa kodi, iweje Rais wa nchi ndogo kama Tanzania. Wameifungia Mwananchi kwa kutaja viwango vya mishahara ya watumishi wa Umma. Wamfungie Mbunge kama wanaweza. --- Zitto Kabwe.
Akizungumza katika mkutano wake mjini Mpanda jana wilayani Sikonge wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika ziara ya Kanda ya Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa chama, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe  ameutaja mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  kuwa ni jumla ya shilingi milioni 26 pasipo
kukatwa kodi. Akichanganua alisema Pinda anapokea sh. mil. 11.2 kama mbunge, sh mil. 8 kwa nafasi ya Waziri na kiasi kinachosalia  kufikia sh mil. 26 kwa nafasi ya Waziri Mkuu.

Alisema sababu hiyo ya mishahara mikubwa isiyokatwa kodi ndiyo huwafanya viongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakali pale vyombo vya habari vinapotaka kuwafahamisha wananchi namna watumishi wao wanavyojilipa.

“Nimeanza na mshahara wa Waziri Mkuu pia siku zijazo nitataja na wa Rais, kwa kuwa amesaini makubaliano na Serikali ya Marekani kuendesha nchi kwa uwazi, na moja ya uwazi ni kwa muajiri kujua kiasi anachomlipa mwajiriwa wake,” alisema Zitto.

Hatua ya Zitto imekuja baada ya kuwapo mvutano mkubwa kuhusiana na kile kinachodaiwa ‘usiri’ wa mishahara ya watumishi wa umma, wakati ni haki ya walipa kodi kujua kile wanachowalipa walioomba kuwaongoza. (nukuu kutoka TanzaniaDaima)


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU