Facebook Comments Box

Wednesday, September 25, 2013

TAARIFA: UKWELI KUHUSU AJALI YA SHEIKH NURDIN KISHKI

                    Sheikh Nurdin Kishki
UKWELI KUHUSU AJALI YA SH. NURDIN KISHKI.
Katika Surat Hujurat (49:6) Allaah anasema "Enyi mliyoamini! Akikujieni mpotovu na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutokujua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyoyatenda".
Leo majira ya asubuhi Sh. Nurdin alipokuwa akielekea katika moja ya shule anazozisimamia iitwayo AL-HIKMA BOYS HIGH SCHOOL iliyopo Mikwambe - Kigamboni (Dar es salaam), gari aliyokuwa amepanda iligongana na gari nyingine. Lakini alhamdulillah Sh. Nurdin hakuumia sana.
Baadae aliwahishwa hospitali na vipimo vinaonyesha kuwa hakuumia sana kama inavyozushwa kwenye mitandao hivi sasa.
Sh. Nurdin Kishki anaendelea vizuri na wala msije mkadanganyika na taarifa itakayokuwa tofauti na hii.
Tunamuomba Allaah amkinge Sheikh wetu Sh. Nurdin Kishki pamoja na Masheikh wengine na kila aina ya mabalaa!
'Amin'


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU