Ile operesheni ya
kuwatimua wahamiaji haramu nchini Tanzania imeanza kutekelezwa ambapo
juzi na jana, watu 1851 walikamatwa katika mikoa ya kandoni mwa maziwa
Nyanza na Tanganyika ndani ya siku moja.
Operesheni hiyo pamoja na mengine inalenga kufukuza majambazi, majangili, pamoja kukamata silaha zinazosadikiwa kutumika katika matendo ya kihalifu nchini. Baadhi ya watu walisalimisha silaha zao huku wengine wakiziacha kwa wenyeji.
Mkuu wa Operesheni hiyo kubwa kuliko zote zilizowahi kufanyika nchini Tanzania, iliyopewa jina la,

“Operesheni Kimbunga”, Naibu Kamishina wa Polisi, Simon Sirro amewaasa wananchi kuwa makini na ‘kurithishwa’ silaha hizo kwani ni kinyume na sheria na inawezekana silaha hizo zikawa zimehusika katika vitendo vya kihalifu na hivyo kumsababishia ‘mrithi’ kushitakiwa kwa mujibu wa sheria.
Kuhusu malalamikao ya kutengwa kwa familia za baadhi ya wenyeji na wahamiaji waliooana, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe amesema wengi wa walioondoka kwa hofu hawakuwa na ufahamu kuhusu sheria na hivyo amewataka kuwafike kwenye ofisi za Uhamiaji ili wapatiwe hati za utambulisho na kuishi nchini zitakazotumika kwa muda wa miaka 2 wakisubiri taratibu za kuwapatia uraia.
Mwezi Julai tarehe 29, Rais Kikwete alitoa wito kwa wahamiaji wote haramu waondoke nchini ndani ya siku 14 ambapo ilitarajiwa wangeondoka zaidi ya 50,000 lakini hadi sasa wameondoka 11,600 tu
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog