Mama mzazi wa mtoto aliyechomwa moto ELESIA MWASILE[41] akipelekwa kituoni na wanausalama |
Hapa wanausalama na mama mzazi wa mtoto huyo wakielekea kumwona mtoto huyo katika hospitali ya Rufaa Mbeya |
Baada
ya kukamatwa mama huyo katili alkabidhiwa kwa Dawati la Polisi Jinsia
na watoto chini ya Kiongozi wa Wilaya D\SSGT PUDENSIANA BAITU akimjulia
hali mtoto Emilly
Wimbi la ukatili dhidi ya watoto bado limezidi kuchukua sura
mpya baada ya mtoto EMILLY GEORGE[7] Mkazi wa kijiji cha RUANDA wilaya ya Mbeya
kuunguzwa vibaya mikono yote miwili na mama yake mzazi ELESIA MWASILE[41] kwa
maji ya moto kisha kufungiwa ndani kwa siku saba bila matibabu yoyote.
Akiongea huku akitetemeka kwa hofu ELESIA amesema kuwa
chanzo cha cha kumchoma mtoto huyo ni kutokana na malalamiko ya majirani
wakimtuhumu mtoto huyo kujihusisha na vitendo vya wizi vikiwemo wizi wa pesa na
mayai ya kuku.
Tukio la mwisho lililopelekea mtoto huyo hadi kuchomwa ni
pale ilipodaiwa na mama huyo kuwa mtoto aliiba mayai akidai amechoshwa na tabia
za malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa jirani zake.
Baada ya kuunguzwa kikatili mtoto huyo alifungiwa ndani kwa
siku saba bila matibabu yoyote
hali iliyowafanya majirani kuuliza aliko mtoto kutokana na mtoto huyo kutoonekana
mitaani hali iliyopelekea kutolewa taarifa ofisi ya kijiji ili kubaini aliko
mtoto.
Uongozi wa kijiji baada ya kupata taarifa kwa majirani
walifanya upekuzi na kumkuta mtoto amefungiwa ndani huku akiwa na majeraha
makubwa katika mikono yote miwili ndipo taarifa ilitolewa kituo cha Polisi
MBALIZI ambapo mama huyo alikamatwa.
Baada ya kukamatwa mama huyo katili alkabidhiwa kwa Dawati
la Polisi Jinsia na watoto chini ya Kiongozi wa Wilaya D\SSGT PUDENSIANA BAITU
na Mwenyekiti MARY GUMBO ambaye muda wote alikuwa akiangua kilio kutokana na
kitendo alichofanyiwa mtoto na mama yake mzazi.
Hivi sasa mwanamke huyo anahojiwa na Polisi kituo kikuu cha
kati na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na mtoto amelazwa katika
Hospitali ya Rufaa wadi namba tano akiendelea kupatiwa matibabu.
Vitendo vya unyanyasaji vimendelea kukemewa Mkoani Mbeya na
Asasi mbalimbali hasa kwa watoto vikiwemo vya ubakwaji,ulawiti,kazi za ndani na
baadhi ya watoto wamepata ulemavu wa kudumu ikiwemo kupoteza viungo.
CHANZO: MBEYA YETU
|
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog