MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wapinzani wao, Yanga SC sasa wanaanza kukua na kuachana na mambo ya kitoto, baada ya kuleta mshambuliaji kutoka Nigeria, Ogbu Brendan Chukwudi.
Poppe amesema kwamba kwa muda mrefu Yanga wamekuwa kama watu ambao hawajui soka kwa kusikilizia Simba SC inataka kumsajili nani na wao ndiyo wamfuate.
Watani wanaanza kukua sasa; Zacharia Hans Poppe amewapongeza Yanga kwa hatua ya kutafuta wachezaji wao na si kusikilizia Simba SC wanataka kumsajili nani na wa wamfuate
“Kwenye kikosi cha sasa cha Yanga kuna wachezaji wangapi wa Simba, wengi tu, yule Barthez (Ally Mustafa), Yondan (Kevin), Chuji (Athumani Iddi) na bado walitaka kuwasajili Amri Kiemba na Shomary Kapombe,”.
“Usisahau Mbuyu Twite ni mchezaji ambaye tulikwishamsajili sisi, wao wakacheza faulo na kumchukua juu kwa juu. Sasa namna hii hatuwezi kukuza soka na ushindani hata wa utani wetu wa jadi,”.
“Lazima Yanga iwe na wachezaji wake na utaratibu pia wa kutafuta wachezaji wake, na sisi tuwe na wachezaji wetu na utaratibu pia wa kutafuta wachezaji wetu,”.
“Ona kama sasa, sisi tumesajili mfungaji bora wa Kombe la Kagame, wao wameleta mfungaji bora wa Nigeria, sasa hawa watu wawili washindane kuzipatia matokeo mazuri timu hizi,”.
Kifaa cha Jangwani; Ogbu Brendan Chukwudi akielekea Jangwani baada ya kuwasili jana usiku Dar es SalaamEndelea kuisoma hapa
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog