WAZIRI Mkuu,
Mizengo Pinda ameonja joto baada ya wananchi wa maeneo ya Mloganzira na
Kwembe Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kulala barabarani kama
njia ya kushikiniza kutekelezewa madai yao. Pinda alikwenda Kwembe
kutuliza mgogoro uliotokana na wananchi kudai fidia za viwanja vyao
vilivyochukuliwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya
cha Muhimbili (MUHAS), ambapo majengo ya kisasa yanatarajiwa kujengwa
katika eneo hilo.
Chuo hicho kinatarajiwa kujengwa mpakani katika eneo hilo la mpakani
kati ya Mlogazira (Pwani) na eneo la Kwembe lililopo Wilaya ya Kiondoni
Mkoa wa Dar es Salaam.
“Tuliweza kwenda Ofisi ya waziri ya ardhi na kupewa mchanganuo ambao
ulikuwa unaeleza juu ya fidia ya ardhi na mazao yote yalipo juu ya
mashamba na nyumba lakini wakati wa malipo tulikwazwa na malipo
kiduchu,” alisema Chole.
“Zoezi zima la ulipaji fidia katika eneo hili lilizungukwa na
uchakachuaji katika ofisi ya Manispaa ya Kinondoni na MUHAS (Chuo cha
Afya Muimbili),” alisema Chole.
Naye Abasi Tamimu, alimtaka waziri mkuu kuangalia suala hilo kwa kina
kwani wananchi wa maeneo hayo wamegeuzwa kafara katika mradi huo.
Akijibu hoja hizo waziri mkuu Pinda, alisema kuwa Serikali imesikia
kilio chao hivyo itaanza kulipa fidia kwa kuwalipa watu 93 ambao hapo
awali walikuwa hawajalipwa.
“Tutawalipa hawa wasiopewa chochote kwanza na nyie mliolipwa Serikali
haiwezi kuwafidia mara mbili labda tuangalie utaratibu wakulifanyia
kazi ombi lenu hilo la kupewa viwanja hivyo ngoja nikae na watendaji
wangu kisha nitawaletea jibu,”alisema Pinda.
Aliongeza kuwa katika hilo serikali itamua kutumia ubinadamu hili
kuweza kupunguza matatizo ya wakazi hao na kuhahidi kushughulikia madai
ya uchakachuzi wa fedha kwa wale wote wenye vielelezo.
Hata hivyo wananchi hao waliridhishwa na majibu ya waziri mkuu,
wakisema kuwa hawana jambo jingine zaidi ya kusibiri utekelezaji wa
kauli ya Pinda kwa kuwa ni kiongizi wa juu serikalini.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana,
na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog