Aliyewahi kuwa mgombea wa Uchaguzi Mkuu Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) uliosimamishwa na Fifa, Michael Wambura, amesema
hatashiriki tena kwenye uchaguzi ujao wa shirikisho hilo, Oktoba 27.
Awali Wambura, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa FAT
(sasa TFF), aliwania nafasi ya Makamu Rais katika uchaguzi
uliosimamishwa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa), kutokana na
kuwepo malalamiko kutoka kwa watu walioenguliwa akiwamo yeye.
Jana TFF ilitangaza majina ya wagombea 58 wote
ikiwa ndiyo siku ya mwisho kurejesha fomu, lakini bila kuwepo kwa jina
la Wambura ambaye alipoulizwa na Mwananchi sababu ya kutogombea tena
alisema: “Siwezi kujisafisha na majitaka.”
“Nimeamua kupumzika, nilipigania haki imepatikana
kwa kamati mbili kuundwa. Bila mimi kamati hizo zisingekuwapo, lakini
jambo muhimu ni kwamba siwezi kujisafisha na majitaka,” alisema Wambura.
“Mfumo wa uongozi TFF ni mbovu, kumejaa siasa za
majitaka, hizo kamati zilizoundwa hazitafanya kazi kwa vile tu Wambura
hayupo, ningekuwepo zingepata kazi ya kufanya,” alitamba Wambura.
Nafasi ya Makamu wa Rais inawaniwa na Iman Madega,
Ramadhan Nasib na Walace Karia, huku wajumbe waliomba kuwakilisha
kanda mbalimbali ni Abdallah Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Magati, Mugisha
Galibona, Vedastus Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra Swai, Mbasha
Matutu, Stanslaus Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Mbise na Omari Walii. ni
Ahmed Mgoyi, Yusuf Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius
Kilungeja, Ayoub Nyenzi, Cyprian Kuyava, David Lugenge, Elias Mwanjala,
Eliud Mvela, John Kiteve, James Mhagama, Kamwanga Tambwe na Stanley
William Lugenge, Athuman Kambi, Francis Kumba, Zafarani Damoder.
Charles Komba, Hussein Mwamba, Stewart Masima,
Farid Nahdi, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, Riziki Majala, Twahil Twaha
Njoki, Davis Mosha na Khalid Mohamed. Alex Kamuzelya, Juma Pinto,
Muhsin Balhabou, Omar Abdulkadir, Shaffih Dauda na Wilfred Kidao. Kwa
upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili Hamad
Yahya (Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).Walioomba
nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto Muzo, Michael Kaijage, Omari
Mwindadi, Salum Rupia na Silas Magunguma.
CHANZO:SHAFFIH DAUDA
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog