PICHA NA MAKTABA:
Kocha
 Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amewaita kambini wachezaji 24 kujiandaa 
kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa 
Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
Wachezaji
 hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 
kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
 Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.
Makipa
 walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Huru), Mwadini Ali (Azam), 
Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris 
(Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub 
(Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David 
Luhende (Yanga).
Viungo
 Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu 
Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo 
(Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga),
 John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi 
ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) 
na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
CHANZO:TFF
CHANZO:TFF
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog