Takriban
watu 175 wamefariki mpaka sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo
kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Moto huo
uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo
walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha
raia wengi bila makaazi pamoja na stima.
Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto huo, Tayari Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.
Mlipuko
huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi
katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.
Rais wa Ghana, John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena. Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu, Accra alipotembelea eneo la tukio.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog