Facebook Comments Box

Tuesday, August 27, 2013

CCM WAMFUKUZA UWANACHAMA MBUNGE WAO

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, mjini Dodoma leo mchana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.


 HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemaliza kikao chake cha siku tatu chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ikiwa imeridhia mapendekezo kadhaa ya Kamati Kuu ya CCM, ikiwemo kumfuta uongozi Mbunge wa jimbo la Mjini Magharibi, Zanzibar, Mansor Yusuf Himid. 

 Kufuatia hatua hiyo, CCM itatoa taarifa kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi kuondoa udhamini wake kwa mwanachama huyo kama Mjumbe wa Baraza hilo kwa jimbo la Kiembesamaki.

 Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuia za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

 Hatua hiyo itamfanya Spika wa Baraza hilo kutangaza kiti cha jimbo hilo kuwa wazi na kuitishwa uchaguzi mdogo wa kugombea nafasi hiyo.

 Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa Daud, Ismail akizungumza na Zenji FM radio amesema kikao hicho kimefikia uamuzi huo baada ya kupokea madai ya mkoa wa Magharib kutaka mwanachama huyo afukuzwe kwa madai ya kupinga sera ya Serikali mbili ya Muungano inayoungwa mkono na CCM. 

 Hata hivyo Himid ambaey pia ni mjume wa kamati ya maridhiano Zanzibar, endapo hajaridhishwa na uamuzi wa kufukuzwa kwake anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo.

 Himid aliwahi kuwa Waziri asiekuwa na Wizara ya Maalum katika awamu ya saba ya uongozi inayongozwa na Dk Ali Mohammed Shein. Pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo kabla ya kuwa Waziri wa Maji Ujenzi, Nishati na Ardhi katika Utawala wa rais Amani Abeid Karume. 

Himid alionekana kichocheo kutaka kuliondoa suala na mafuta na gesi asilia kwenye orodha ya Mambo ya Muungano pamoja na kuchukizwa na matatizo ya Muungano yanayoikandamiza Zanzibar. 

Hivi karibuni mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Mzee Hassan Moyo alisema kufukuzwa kwa Himid hakutathiri shughuli za Kamati hiyo katika kutetea Muungano wa mkataba. 

UTEUZI 

 Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuiya za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). 

 Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa UVCCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi. 

Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa. 

Pia, NEC imeridhia mapendekezo ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo. 

 Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha Uchaguzi, CCM Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita). 

Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.

 Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera. 

 Taarifa Rasmi ya CCM ya majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa na NEC 

Ndugu Ashura Amanzi 
Ndugu Rukia Saidi Mkindu
Ndugu Elias J. Mpanda
Ndugu Jonathan M. Mabihya 
Ndugu Mulla Othman Zuberi 
Ndugu Jumanne Kapinga
Ndugu Ali Haji Makame
Ndugu Jacob G. Makune 
Ndugu Juma A. Mpeli
Ndugu Hawa Nanganjau
Ndugu Abdulrahman Shake 
Ndugu Subira Mohamed Ameir 
Ndugu Abdallah Shaban Kazwika 
Ndugu Juma Bakari Nachembe 
Ndugu Josephat Ndulango 
Ndugu Rajab Uhonde
Ndugu Abeid Maila 
Ndugu Mohamed Lawa 
Ndugu Mariam Sangito Kaaya 
Ndugu Bakar Lwasa Mfaume 
Ndugu Julius Peter 
Ndugu Jumanne Kitundu Mginga 
Ndugu Mathias Nyombi 
Ndugu Mohamed Hassan Moyo


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU