Facebook Comments Box

Friday, June 21, 2013

WAKE WA MARAIS KUFANYA MKUTANO TANZANIA MWEZI UJAO


Mke wa Rais wa Marekani,Michelle Obama, 
Dar es Salaam. Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush na mkewe,Laura wanatarajiwa kuendesha Mkutano wa Kimataifa wa wake wa marais wa Afrika kuzungumzia nafasi ya wanawake kuinuka kimaendeleo utakaofanyika Dar es Salaam, Julai 1-2 mwaka huu.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini, utakwenda sambamba na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama pia utajumuisha maofisa wa Serikali,viongozi wa mashirika ya kiraia na wasomi wa kada mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Wakfu wa George W. Bush imesema kuwa mkutano huo utakaokuwa na kauli mbiu; “Kuwekeza kwa wanawake kunaiinua Afrika” imewataja baadhi ya wazungumzaji kuwa ni pamoja na Bush mwenyewe na mkewe Laura, Mke wa Rais wa Marekani,Michelle Obama, Mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza,Cherie Blair na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi (Unaids), Michel Sidibé.
Taarifa hiyo imesema kuwa wake hao wa marais wa Afrika wanatoa mchango mkubwa wa kusukuma mbele agenda za maendeleo katika sekta za afya na elimu hivyo kukutana kwao kutatoa fursa nyingine ya kujadiliana changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya pamoja.
“Wake za marais wanalo jukumu muhimu kuhusiana na uboreshwaji wa ustawi wa wanawake… wao wana nafasi kubwa ya kuinua na kuboresha sekta kama elimu,afya na maendeleo ya kiuchumi hivyo kukutana kwao ni hatua muhimu itayotoa mwanga kuhusiana na hatua zinazopaswa kufanywa kuwawezesha wanawake,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Baadhi ya wake za marais watakaohudhuria mkutano huo ni wa pamoja na Mke wa Rais wa Uganda, Janet Museveni,mke wa Rais wa Msumbiji, Maria da Luz Dai Guebuza, mke wa Rais wa Sierra Leone, Sia Nyama Koroma na mwenyeji wao Salma Kikwete.
Miongoni mwa mada zinazotarajiwa kujadiliwa wakati wa mkutano huo ni pamoja na kuwawezesha wanawake ujasiriamali kupitia mafunzo ya teknolojia,kutoa fursa na kuboresha shughuli za kilimo kwa wakulima wanawake na ukoaji wa maisha kwa kukabiliana na saratani ya ziwa


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU