Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, imevikataza vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Madiwani kwenye Kata nne za Arusha Mjini, kufanya kampeni katika kipindi hiki ambacho uchaguzi huo umehairishwa hadi Juni 30 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, JULIUS MALLABA amesema kwamba sheria za uchaguzi haziruhusu kwa sasa vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuwa uchaguzi katika Kata hizo umeahirishwa baada ya muda wa kampeni ulikwisha.
Vyama ambavyo vitaonekana kukiuka taratibu hizo vitachukuliwa hatua na kamati za maadili ambazo zinajumuisha wajumbe kutoka vyama vyote vya siasa nchini.
MALLABA pia ametoa wito kwa wananchi wa Kata hizo nne -- Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai -- kuwa ifikapo siku ya kupiga kura, washiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog