“PRESS RELEASE” TAREHE 11. 06. 2013.
WILAYA YA MBOZI -
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA
VIFO.
MNAMO TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO ENEO LA
ILOLO VWAWA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.840
BKD AINA YA TOYOTA HARRIER LIKIENDESHWA NA DEREVA BROWN S/O MWAKIBAMBO,MIAKA
34,KYUSA, MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MARIAM D/O HALINGA,MIAKA
27,MKULIMA MKAZI WA ILOLO AKIWA AMEMBEBA
MTOTO WAKE AITWAE HELENA D/O SAMSON,UMRI
WA MWAKA MMOJA NA NUSU, KYUSA NA
KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI . TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA KYELA - KUINGIA
NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 01:30HRS HUKO KATIKA
NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO GWAKISA ENEO LA KYELA - KATI WILAYA YA KYELA
MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. LUKINDO S/O JOHN,MIAKA 45 NA 2. MSEMAKWELI S/O JOHN, MIAKA 27 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI
RWANDA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUSAFIRI KWA
KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA
KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI HATUA ZA
KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI
PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog