Waumini
 wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye Kongamano lililofanyika leo jijini 
Dar es Saalaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mada mbalimbali 
ziliwasilishwa na masheikh. Msimamo wa waisilamu juu ya Maendeleo ya 
mchakato wa katiba mpya, Dhulma na uonevu dhidi ya waislam pamoja na 
hatua za kuchukuwa kama madai yao yatapuuzwa.       
 
Waumini wa dini ya Kiislam leo
 wametoa msimamo juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini wakati 
wa kongamano lililoandaliwa na jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania 
jijini Dar es Salaam. 
 
Kwenye
 kongamano hilo ambalo masheikh mbalimbali wakiwemo Sheikh Ponda Issa 
Ponda, Ally Basaleh, Mussa Kundecha na Kondo Juma Bungo waliwasilisha 
mada mbalimbali pamoja na kutangaza maazimio ya kongamano hilo. 
 
 
Moja
 ya mambo yaliyozungumzwa ni mapendekezo waliyowasilisha kwenye Tume ya 
katiba mpya ambapo walisema iwapo mapendekezo waliyowasilishwa 
hayakuzingatiwa na kutupwa yote basi waisilamu watatangaza kusimamisha 
mchakato huo nchi nzima na kufanya maandamano usiku na mchana. 
 
Hoja
 hiyo ilikuja baada ya kunukuliwa kauli ya Waziri wa nchi Sera na 
Uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi, wakati akijibu swali la Mbunge Asumta 
Mshama aliyetaka kujua kwamba lini serikali itaacha kupanga siku ya 
kupiga kura kuwa Jumapili wakati wanajua siku hiyo ni siku ya ibada ya 
wakristo haioni inawadhulumu hakiyao yakufanya ibada?, Lukuvi kwenye 
jibu lake alisema suala hilo limekuwa likilalamikiwa na watu wengi tu 
lakini serikali kwenye hilo haina utaratibu maalum wa siku ya kupiga 
kura ila kwakuwa kuna mchakato wa katiba mpya hilo litazingatiwa. 
 
 
“Hii
 ni kinyume kabisa na utaratibu wa tume ya katiba waziri huyu anataka 
tuamini kwamba  anayafahamu yatakayokuwemo kwenye katiba mpya kabla hata
 wananchi hawajapelekewa na hata haijaandikwa? Hivyo iweje waislam 
wanaodai siku ya ijumaa iwe ya mapumziko kwa miaka nenda rudi hawapewi 
wakristo wanakosa sikumoja tu ndani ya miaka mitano majibu yanapatikana 
kirahisi?” Alihoji sheikh Ponda. 
 
 
“Waislam wamekuwa wakiomba ruhusa kwa mabosi wao siku ya ijumaa kwenda 
kufanya ibada na mara nyingine wananyimwa ruhusa hiyo lakini hakuna 
vurugu yeyote waliofanya na wanadai haki hiyo kwa miaka yote hii lakini 
hawapewi lakini wengine wanadai kirahisi na kujibiwa kwa uhakika.” 
Alifafanua. 
 
 
Aidha
 heikh Ponda alifafanua kuwa waislam wavumilie wasubiri rasimu 
itakapotangazwa kwenye magazeti ya serikali kama mapendekezo 
waliyowasilishwa yatapuuzwa basi hakuna katiba mpya maandamano usiku na 
mchana mpaka kieleweke nchi nzima. 
 |