Facebook Comments Box

Sunday, June 2, 2013

MAMA YAKE 'NGWEA' ADONDOKA GHAFLA NA KULAZWA HOSPITALI


            Bi Denisia Mangwea.mama mzazi wa msanii Albart Mangwea
 
 Mama mzazi wa  marehemu Albart Keneth Mangwea 'NGWEA' Bi Denisia Mangwea[63] leo asubuhi ameanguka ghafla baada ya kupokea taarifa kwamba mwili wa mtoto wake Albeth umeshindwa kuwasili nchini ukitokea Afrika ya kusini.Mtandao huu leo mchana ulipokea taarifa z a tukio hilo  ambapo dada mkubwa wa Albeth Bi Magreth Mangwea alipoulizwa alithibitisha mama yake kuanguka ghafla baada ya kusikia mwili wa mpendwa mtoto wake umeshindwa kuwasili  nchini.
 
" Ni kweli leo asubuhi mama alipoamka na kusikia taarifa kuwa mwili wa mwanae hautofika tena leo Jijini Dar es Salaam kutokana na Taarifa ya Daktari kuchelewa kutolewa  alianguka kwa presha na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akiendelea na matibabu, na alizinduka baadae  na anaendelea vizuri na kwamba muda wowote anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU