Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi ya watu wamejitolea vyombo binafsi vya usafiri na wengine wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa hospitali hizo kutoa huduma ya kwanza.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo.
Bomu hilo linaelezwa kuwa lilipuka kwenye mkusanyiko wa watu meta chache kutoka jukwa kuu, mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo hilo.
Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA. Mwandishi mmoja wa habari anaripotiwa kunyang’anywa kamera yake baada kwa kupiga picha, hata baada ya kujitambulisha.
Watu wenye hasira wanaripotiwa kuyashambulia na kuyaharibu baadhi ya magari ya kutoa huduma ya kwanza (ambulance) kwa kuwa yalichelewa kufika kuwaokoa majeruhi.
ILANI: Baadhi ya picha zilizopachikwa hapo huenda zikagusa hisia ya mtizamaji, tafadhali ikiwa huwezi kuvumilia kuona damu usibofye kitufye cha kuelekea mbele
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog