Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali yake inawatambua watu
walioshirikiana na Jumuiya ya Uamsho kuanzisha vurugu za kisiasa na
kuacha kufanya kazi za kiroho kinyume na malengo ya kusajiliwa kwa
jumuiya hiyo visiwani Zanzibar.
Dk Shein Akihutubia mkutano wa
hadhara, Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, alisema jumuiya ya Uamsho
iliwalazimisha polisi kutumia nguvu baada ya serikali kuwakanya na
kuwaonya zaidi ya mara tatu wasitishe vurugu zao.
Alisema Serikali ina mikono mirefu na tayari imekwishawafahamu wote
walioandaa mpango wa vurugu kwa kusingizia kero za Muuungano na wakati
ukifika haitosita kuwachukulia hatua za kisheria ili kulinda amani na
umoja wa kitaifa Zanzibar.
Alisema kifungu cha 19 (1) cha
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kimesema kila mtu anastahili kuwa na
uhuru wa mawazo, wa imani na wa uchaguzi katika mambo ya dini pamoja na
uhuru wa kubadilisha dini au imani yake bila ya kuingiliwa.
Alisema endapo yakizuka matatizo mengine yenye kutishia amani ya nchi
Serikali yake itawatafuta wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za
kisheria.
Kitongoni katika mahojiano yake na baadhi ya watu dhidi ya hotuba hiyo ya Mh Rais wengi walikuwa wanahoji kwanini serikali isiwakamate hao waliopanga vurugu au inasubiri mpaka vurugu zifanywe na watu wadhurike? Wengine walikuwa wakihoji uhuru wa kutoa maoni wa wananchi unaishia wapi? Kuna mambo wananchi hawapaswi kuyajadili?
Mwanasheria mmoja alieongea na Kitongoni yeye kwa maoni yake alisema Mh Rais anaiingilia uhuru wa mahakama kwa kuzungumzia mambo yaliyopo mahakamani na yakisubiri hukumu. "hotuba ya Mh Rais inaweza kumshawishi Hakimu au Jaji katika maamuzi yake."
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog