Facebook Comments Box

Monday, May 20, 2013

HATIMAYE MBUNGE WA IRINGA MJINI AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mh Msigwa akishuka kwenye gari la polisi kuingia mahakamani
Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji,  Peter Msigwa akishuka katika gari ya  polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana  huu katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa  wa Iringa  pamoja na  watuhumiwa  wengine  zaidi ya 60 .
 
Ulinzi mkali uliwekwa katika eneo hilo la mahakama  kuzuia wafuasi  wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuingia eneo la Mahakama jambo lililowafanya wafuasi hao kushindwa kushuhudia vyema kesi hiyo, inayomkabiri Mbunge wao, kwa vile walilazimika kushuhudia wakiwa nje ya geti

 Kada wa Chadema Frank Mwaisumbe akiingia na viongozi  wengine wa chadema mahakamani hapo huku  wafuasi  wao  wakizuiwa nje ya mahakama
 Wafuasi  wa Chadema  wakiwa  wamezuiliwa nje ya viwanja  vya mahakama kuu kanda  ya Iringa  wakati mbunge  alipofikishwa katika mahakamani   mchana  huu


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU