Facebook Comments Box

Tuesday, May 21, 2013

AZAM TV KUONESHA LIGI KUU YA TANZANIA BARA MSIMU UJAO WA 2013/2014



Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) inayomiliki klabu tajiri ya Azam FC ipo mbioni kumwaga zaidi ya 1.5 bilioni kwa timu zote za ligi kuu Bara msimu ujao na itarusha moja kwa moja (Live) zao kupitia televisheni yao mpya ya AZAM TV ambayo inatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni ambapo ujenzi wa kituo hicho unaendelea katika Jengo moja lililopo Barabara ya Mandela, Jijini Dar es Salaam.

Habari za uhakika zinasema Azam itauza Ving'amuzi na inakusudia kutoa kiasi cha shilingi Milioni 100 kwa kila timu kwa timu zote 14 zitakazo shiriki ligi kuu msimu ujao na Mkataba huo utakuwa ni wa miaka mitano (5). Kamati ya ligi chini ya Wallace Karia na viongozi wa TFF walikutana na klabu za ligi kuu kujadili mkataba huo ambao utazipunguzia mzigo klabu ndogo ambazo zimekuwa zikisumbuliwa na ukata kutokana na kutegemea udhamini wa Vodacom pekeyake ambao hautoshi.




Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU