Facebook Comments Box

Wednesday, April 3, 2013

VURUGU ZATOKEA TUNDUMA JUU YA NANI ACHINJE

Ghasia zinazoendelea katika mji wa Tunduma ulioko mkoani Mbeya zimechochea uharibifu kijamii. Tunduma haiko katika hali nzuri.
 Vurugu kama hizo ziliwahi kutokea mjini Mwanza na kuhusisha wamumini wa imani ya kikristo na Kiislamu. Mauaji yalitokea na serikali ilifanya juhudi kuwakamata wahusika.

Ni kwamba inaelekea hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu uchinjaji bado haijaeleweka, hivyo wakristo bado walikuwa na msuguano na wenzao juu ya nani achinje.

Tamko la Polisi lilisema waislamu waendelee kuchinja sasa leo alfajiri vijana wa kikristo walienda machinjoni na kumgawia kichapo cha kutosha mchinjajiwa kiislam ambaye alifanikiwa kutoroka.

Baada ya hapo wakristo nasikia ndiyo wakaanza hizo fujo ikiwemo pamoja na kufunga barabara, kuharibu msikiti, kubomoa nyumba ya polisi mmoja aliyejenga uraiani, wameandamana na biblia mikononi kudai haki ya kuchinja.

Polisi wa Tunduma kazi imewaelemea na ikabidi nguvu itoke mkoani na RPC yupo huko sasa hivi. Juzi kanisani Padre mmoja alitoa kauli kuwa kama hawa watu wanataka kuchinja basi watuchinjie na kitimoto.

Raia ilibidi wakimbilie mahakamani kwa kuona kwamba ndiyo sehemu pekee ya usalama kwao, hivyo ikalazimu mahakama kuhairishwa ili kuepusha balaa. Kale kamchezo kakuchoma matairi na kufunga barabara kakawa ndiyo mchezo wa kawaida.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU