Timu zinazoshiriki ligi kuu ya
England zinatarajiwa kukubaliana kupitisha matumizi ya teknolojia ya
mstari wa Goli maarufu kama GOAL LINE TECHNOLOGY baadaye wiki hii ambapo
taarifa toka kwenye chama cha soka cha England imesema kuwa klabu hizo
zimezungumzia suala la matumizi ya teknolojia hiyo na zitakutana tena
siku ya alhamis ambapo agenda kuu ya mkutano huo inatarajiwa kuwa
makubaliano ya kupitisha matumizi ya teknoljia hiyo kwenye michezo ya
ligi kuu ya England kuanzia msimu ujao.
Kampuni ambazo zimeingia kwenye
mashindano ya kuwania tenda ya ufungaji wa teknolojia hiyo kwenye
viwanja vya ligi kuu ya England ni Kampuni ya HawkEye,Cairos,Goalcontrol
na Goalref ambapo teknolojia hiyo itaanza kutumika kwenye mchezo wa
ufunguzi wa ligi kuu ya England ambao ni mchezo wa kuwania Ngao ya jamii
unaochezwa kati ya mshindi wa ligi kuu na mshindi wa kombe la Fa,
tayari shirikisho la mchezo wa soka ulimwenguni FIFA limepitisha
matumizi ya Goal line Technology ambapo teknolojia hiyo itaanza
kutumika kwenye michuano ya kombe la mabara.
Chama cha soka cha England
tayari kimepitisha matumizi ya teknolojia hiyo kwenye uwanja wake wa
Taifa wa Wembley na kimeanza kupitia mapendekezo mbalimbali toka kwenye
makampuni yanayofunga mifumo ya teknolojia hiyo.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog