Mwisho wa Kubadili leseni za madereva umeongezwa mpaka April 30, 2013 badala ya march 31, 2013 ya awali. Muda huo uliongezwa baada ya kikao ambacho Polisi walikaa pamoja na Mamlaka ya mapato kujadili kutokana na matatizo ambayo yalijitokeza na kusababisha madereva kushindwa kubadili leseni hizo kwa wakati. Moja ya sababu hizo ni Mtandao kuwa chini kwa muda mwingi.
Kamanda Mohamed Mpinga amesema muda huo wa mwezi mmoja ulioongezwa unatosha na hakutakuwa na muda mwingine tena na Dereva atakayeshindwa kubadili leseni ya zamani na kuchukuwa mpya atafikishwa mahakamani mara moja kujibu shitaka atakalo kuwa amepelekwa nalo la kushindwa kubadili leseni yake kwa wakati.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani – SACP. Mohammed R. Mpinga (kushoto) na Mr. Salum Yusuph -
Naibu Kamishna wa Kodi za ndani TRA (kulia) wakisikiliza maswali
mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari (pichani hawapo) kuhusu mwisho
wa kubadili leseni za zamani za udereva utakao kuwa mwisho wa mwezi huu
30/04/2013.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog