Chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro (Mum),
kimeanzisha uhusiano wa kitaaluma na Chuo Kikuu cha Osman Dan Dodio
Sokoto (Udus) cha Nigeria.
Makubaliano hayo yalifikiwa kati ya ujumbe wa Mum ulioongozwa na Kiongozi wa Baraza la Chuo, Ahmed Saggaf na Sultan wa Sokoto, Alhaji Muhammad Sa’ad Abubakar III. Pia, ujumbe wa Mum ulijumuisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Kassim Umba na Mhadhiri wa chuo hicho, Faraj Tamim.
Taarifa iliyotolewa na Baraza la Mum, inasema lengo la ziara hiyo ni kuanzisha uhusiano kati ya Chuo Kikuu cha Osman Dan Fodio Sokoto (UDUS) na Chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro (Mum).
Inasema ushirikiano huo utahusisha programu kubadilisha wahadhiri na wanafunzi, kubadilishana uzoefu kwenye masomo ya Sharia, udaktari, jiolojia na utoaji nafasi za masomo. UDUS kina wanafunzi 35,000.
Vilevile uongozi wa MUM ulimuahidi Sultani wa Sokoto, Alhaj Muhammad Sa’ad Abubakar III kuendeleza ushirikiano huo, huku Sultan akielezea kufurahishwa kwake na mwaliko wa kutembelea Tanzania ambayo imekuwa ikisifiwa duniani kwa umoja na amani.
Pia, Sultan alishukurua uongozi huo kwa kutembelea Sokoto na kwamba, kutokana na juhudi hizo zimeweza kuunganisha vyuo hivyo
SOURSE: MWANANCHI
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog