Taarifa rasmi kutoka kwenye uongozi wa Simba ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba Kaburu leo ametuma barua pepe kwenda kwa mwenyekiti wa klabu ya Simba Mh.Aden Rage akimuelezea maamuzi yake ya kujivua madaraka ya kuitumikia Simba kutokana mgawanyiko mkubwa uliopo kwenye uongozi wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari Kaburu ameelezea kwamba kamati ya utendaji imegawanyika na ufa uliopo hautoi nafasi nzuri kwake kuitumikia vizuri Simba, akisema ni moja ya sababu ya timu yao ya Simba kutofanya vizuri katika michuano mbalimbali inayoshiriki.
Pia Kaburu amesema amechukua maamuzi hayo ni njia mojawapo ya kuwajibika kama kiongozi kutokana mambo kutokwenda vizuri hali ambayo imesabababisha kutukanwa na kupigiwa kelele nyingi na wanachama na wapenzi wa Simba SC Mwenyekiti. Hivyo ameamua kujiuzulu kupisha wanachama wengine wa Simba waweze kuliongoza jahazi la klabu hiyo.
Katika hatua nyingine mwenyekti
wa kamati ya usajili na mjumbe ya kamati ya utendaji Zacharia Hans Pope
nae ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi zote alizokuwa akishikilia
Simba.
Pia kwenye taarifa yake ya
kujiuzulu Pope amesema mgawanyiko uliopo kwenye uongozi ndio chanzo cha
kujiuzulu kwake katika kuitumikia Simba kupitia nafasi za uongozi
alizokuwa nazo kwa takribani miaka 3.
SOURSE: SHAFFIH DAUDA
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog