Facebook Comments Box

Friday, March 29, 2013

DIAMOND NA WEMA WATAMBIANA KATIKA PESA

Wakati WEMA ISACK SEPETU akifungua bonge la ofisi ya kuzalisha filamu, aliyekuwa Mpenzi wake Nasibu Abdul 'DIAMOND PLATNUM' amemjibu kwa kukamilisha mjengo wa maana uliomgharimu takriban Shilingi za Kitanzania Milioni 260 hivyo kwa pamoja kuonesha jeuri ya pesa walizo nazo.

WEMA alifanya uzinduzi wa ofisi yake hiyo bila kumpa taarifa Mama yake mzazi MARIAM SEPETU ili iwe bonge la Surprise kwake pamoja na watu mbalimbali kama vile Diamond Platnumz mwenyewe siku ya Jumatano iliyopita, Jina la Ofisi hiyo ni ENDLESS FAME FILMS iliyopo Mwananyamala- Komakoma Jijini Dar es Salaam.

Wema akiwa katika Ofisi yake hiyo Mpya ya Filamu
Wema akiwa Nyumbani kwake.
Wema akitoka kwake na gari yake aina ya Audi Q7.

Pamoja na Diamond kutoalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Ofisi hiyo ya Wema lakini chanzo cha habari kinasema alikuwa katika harakati za kumalizia Mjengo wake ulioko Tegeta ili nae afanye uzinduzi rasmi. Akizungumza na kitongoni blog akiwa kwenye eneo ilipo nyumba hiyo ambayo ilikuwa ikifanyiwa ‘finishing’, Diamond alisema kuwa nyumba hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 260 ni zawadi kwa mama yake SANURA KASSIM ‘SANDRA’.

“Mama yangu ndiyo kila kitu kwangu, mara ya kwanza nilimnunulia gari aina ya Toyota Alteeza nikaona haitoshi, nikaamua kumjengea hii nyumba ambayo itakuwa kama urithi wake hata nikifa leo,” alisema Diamond.

Diamond alimzungusha paparazi wetu na kujionea mjengo huo wenye vyumba vinne vya kulala ambavyo vyote ni ‘self contained’ (chumba chenye choo na bafu), studio kubwa ya kurekodi muziki, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kujenga bwawa la kuogelea ‘swimming pool’, uwanja wa basketball na sehemu maalum ya kufanyia mazoezi (gym) ambapo alisema hadi ifikapo Septemba, mwaka huu kila kitu kitakuwa kimekamilika.
Hii ndiyo Nyumba ya Diamond anayojenga huko Tegeta na gari linalo onekana hapa ndilo gari lake anlotumia ukiachilia mbali Altezza aliyo mnunulia Mama yake.Ukiachana na ukubwa wa nyumba hiyo, uwanja ambao ameuzungushia uzio wa ukuta kuna nyumba nyingine ndogondogo tatu ambazo kwa mujibu wa staa huyo zitakuwa zikipangishwa.
Diamond akiwa Nyumbani kwake Sinza Mori anapoishi sasahivi.







Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU