Facebook Comments Box

Friday, February 22, 2013

PSPF WAONESHA NYUMBA ZAO ZA MKOPO ZILIZOPO BUYUNI - CHANIKA




Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka 2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla.

Mikoa iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam – Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli (50), Tabora – Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).

Aidha kwa Mujibu wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu amewaambia wanandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la mradi huo Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga nyumba za aina nne ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.

Gharama ya ununuzi wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni kati ya Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na Kodi ya ongezejo la Thamani.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba 491 zilizopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo zitkopeshwa kwa wanachgama wa mfuko huo. Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo ya kuakagua makazi hayo. Kulia ni  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Hery Mohamed Kessy Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
 Wadau mbalimbali wakitembelea nyumba hizo hii leo.

 Ziara ikiendelea katika nyumba hizo zipatazo 491




Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU