Facebook Comments Box

Monday, February 4, 2013

PICHA: PAMOJA NA MITI YOTE HII WAFUASI WA CHADEMA NA CCM WAGOMBEA MTI

Picha zilizopachikwa hapo chini kutoka kwenye blogu ya Mpoki aka Mzee wa Sumo zinaambatana na taarifa za tukio hilo kama ilivyosimuliwa kwenye magazeti ya:

MWANANCHI, “Wafuasi CHADEMA, CCM wagombea mti wa bendera” ama  HabariLeo, “CHADEMA wavuruga sherehe za CCM Dodoma” au MTANZANIA, “CCM watoa kichapo kwa vijana wa CHADEMA” na bila kusahau NIPASHE, “MIAKA 36 YA CCM: JK aomba umoja - Vurugu kubwa zaibuka Dodoma.”

Picha moja, tukio moja, maneno elfu na tafsiri hazina budi kutofautiana kulingana si tu mtoa habari, bali pia mpokeaji. Ndiyo maana kabla ya “jury” kufikia maamuzi, na Hakimu kuhukumu, hawana budi kupitia vielelezo vingi iwezekanavyo.

Kuna kauli moja Mzee wa Changamoto, Mubelwa Bandio, ameiweka kama kauli mbiu ya blogu yake inasema, “(may be) The way you see the problem, is the problem.”

Smiley face Smiley face Smiley face Smiley face Smiley face



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU