Facebook Comments Box

Monday, February 4, 2013

MADUKA YATEKETEA KWA MOTO KITUO CHA DALA DALA - MWENGE


 Wafanya biashara na Wasafiri wakiangalia moto ulivyokuwa ukiendelea kuteketeza maduka kituo cha mabasi cha Mwenge, Dar es Salaam.


Maduka yanayozunguka Kituo cha mabasi (dala dala) cha Mwenge leo yameteketea kwa moto mkubwa ambao bado chanzo chake hakijafahamiaka, Pamoja na kuchelewa kufika kwa kikosi cha zimamoto lakini kimefanya jitihada za kuhakikisha moto huo unazimika ili kunusuru mali za wafanyabiashara pamoja na maduka yao.

Kama ilivyo ada vibaka nao waliingia kazini kujihakikishia nao wanpata chochote katika vurugu hizo wakati wananchi wakikimbia ili kuweza kujiokoa na moto mkubwa uliokuwa unawaka katika maduka hayo.

Majanga ya moto yameendelea kulisakama jiji la Dar es salaam kwani ni jana tu jengo la PPF Tower maeneo ya Posta lilinusurika kuteketea baada ya ghorofa ya 17 katika jengo hilo kuteketea kwa moto hata hivyo wadau wa uzimaji moto waliweza kulinusuru.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU